LIVE STREAM ADS

Header Ads

Siri ya Mnadani Fc kuibuka na ubingwa Ndondo Cup Jijini Mwanza yajulikana

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Hatimaye mashindano ya Ndondo Cup 2017 Jijini Mwanza, yamefika tamati kwa timu ya Mnadani Fc kutoka wilayani Ilemela kuibuka mabingwa katika msimu huu wa kwanza baada ya kuichapa Milo Clan (Watoto wa Muji) kwa goli 5-1.

Katika mchezo wa fainali uliochezwa jana kwenye uwanja wa Nyamagana na kuzikutanisha timu hizo, Mnadani Fc walionekana kuwa na mashambulizi zaidi ya wapinzani wao Milo Clan kutoka katika ya Jiji.

Mnadani Fc ilifunga goli kupitia washambuliaji wake, Bernard Isdory aliyefunga hatrick dakika ya 6, 22 na 52 huku Evarist Tembo dakika ya 39 na Yusuph Kilamuhama dakika ya 65 wakati Milo Clan wakipata goli dakika ya 77 kupitia Karim Said Benzema kwa penati na dakika ya 44 mchezaji wa timu hiyo Emmanuel Swita alipewa kadi nyekundu.

Akizungumzia mchezo Kocha Msaidizi wa Milo Clan, Makkah Edu alisema fainali siku zote timu zote uwa zinakuwa na  na mwamko na hamasa kubwa ya kufunga hivyo atajipanga msimu ujao.

Naye mchezaji wa Mnadani Fc, Isdory aliyefunga hatrick katika fainali hiyo alisema mashindano ni mazuri na timu imefanya vizuri kutokana na mazoezi na juhudi binafsi na ataendelea kufanya vizuri zaidi.

Hata hivyo katika mashindano hayo Mnadani Fc ndio imeibuka mabingwa na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, kombe na medani, huku Milo Clan wakishika nafasi ya pili na kuondoka na shilingi milioni mbili na medali na Morning Star ikishika nafasi ya tatu na kupatiwa shilingi milioni moja.

Aidha mchezaji kutoka Milo Clan Karim Said Benzema na  Kheri Khalfan kutoka Phantom FC kuibuka wafungaji bora na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano kila mmoja baada ya kufunga jumla ya magoli 7 tangu kuanza kwa mashindano hayo msimu huu.

Naye  Deus Kazoka kutoka Mnadani Fc aliibuka kipa bora na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na Bruno John kutoka Milo Clan aliibuka mchezaji bora na kupatiwa shilingi laki tano huku mashabiki wa timu ya Morning Star kutoka Kisesa wakiibuka kikundi bora cha ushangiliaji na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.


Naye Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema Mwanza ndio nyumbani kwa Ndondo Cup kwani  imefanya vizuri zaidi ya Dar es salaam ikizingatiwa ni mara ya kwanza lakini wananchi wamekuwa na hamasa kubwa.

No comments:

Powered by Blogger.