LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tamasha la injili "Lakwetu Concert 2017" kutikisa msimu wa Krismas Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Tamasha la "Lakwetu Concert" linatarajia kufanyika msimu wa siku kuu ya Chrismass kuanzia Disemba 24 hadi 26 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Tamasha hilo linaloandaliwa na Farama Promotions  ambalo linafanyika kwa mara ya pili litakua  la tofauti ukilinganisha na mwaka jana kwani limeboreshwa zaidi.

Akizungumza na BMG, mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel alisema msimu huu tamasha hilo litakuwa tofauti kutokana na  kufanyika siku tatu mfululizo tofauti na mwaka jana ambapo lilifanyika kwa siku  moja na kusababisha baadhi ya waibaji kukosa nafasi ya kutumbuiza.

Fanuel alisema kutakua na uzinduzi wa albamu  mbili kwa pamoja, sambamba na utoaji vyeti 100 kwa watu wanaounga mkono muziki wa injili mkoani Mwanza huku wadau watakao  dhamini  tamasha hilo kuongezaka.

Pia alisema washindi wa  Lakwetu Talent Search  kutoka wawili mwaka jana hadi wanne mwaka huu, huku waimbaji zaidi  ya  200 kutumbuiza kwa siku zote, pamoja na wachungaji na Maaskofu mkoani Mwanza kushiriki katika tamasha hilo.

Aidha aliongeza kuwa, kutakua na maombi ya kuombea amani, upendo na umoja kwa nchi na viongozi Tanzania.


Hata hivyo alisema wanatarajia  tamasha hilo kuhudhuriwa na viongozi  wakuu kutoka serikalini na taasisi mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.