Kampeni ya "Amsha Viwanda" yazinduliwa Nyamagana
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Msimamizi
Mkuu wa Shirika la Voluntary Service
Overseas (VSO), Frank Girabi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya amsha
viwanda.
Judith Ferdinand,
Mwanza
Katika kuunga ndoto za Rais za kuwa na uchumi wa viwanda
na kuhakikisha wajasiriamali wanaendelea, Shirika la
Voluntary Service Overseas (VSO) kupitia
mradi wake wa Kuwasaidia na kuendeleza
Wajasiriamali Tanzania (TLED) limeanzisha
kampeni ya Amsha Viwanda.
Kampeni hiyo ambayo
itafanyika katika wilaya nne za mkoa wa Mwanza ikiwemo Nyamagana, Ilemela, Magu
na Kwimba, ambayo imelenga kuhakikisha wajasiriamali wanafanya shughuli zao kwa
uangalizi sambamba na kuunganishwa na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za
kifedha na za serikali, kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Akizungumza jana katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika
wilayani Nyamagana, Msimamizi Mkuu
mradi wa TLED wa
shirika la VSO Frank Girabi alisema,
kampeni hiyo ni sehemu ya
kutekeleza mradi wao ambao unafanyika kwa miaka mitano katika mikoa sita nchini
ikiwemo Mwanza, wakishirikiana na SIDO,TCCIA,TWCC na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Girabi alisema, wamejikita
katika kutoa mafunzo na ushauri,kwani
wanawasaidia wajasiriamali wadogo katika nyanja tofauti tofauti ambazo
wanazokutana na changamoto mbalimbali
ikiwemo soko,usimamizi wa fedha na biashara zao.
Pia alisema, kupitia mradi huo wanatarajia kuwafikia
wajasiriamali 1760 nchi nzima, hasa wakina mama ambao wanatoka katika maeneo
wanawasaidia kwa kuwakutanisha na masoko, kuwapa mafunzo pamoja na kuwapeleka
kwenye fursa mbalimbali zilizopo ndani na nje ya nchi,ili kukuza biashara
zao,kuchangia pato la taifa na kutoa ajira kwa vijana na wengine.
Kwa upande wake Meneja wa
SIDO Bakari Songwe alisema,
kampeni hiyo ni moja ya jitihada ya za
shirika lao kuwasaidia wajasiriamali kwa kuhamasisha katika kuendeleza viwanda
vidogo pamoja kurasimisha bidhaa zao na
ubora, ikiwa ni njia ya kumuunga mkono Rais ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Naye Makamu Mwenyekiti wa
TCCIA Leopard Lema alisema,wajasiriamali wanatakiwa kufanya kazi kwa
bidii,kufuata taratibu za serikali pamoja na kuhudhuria mafunzo na fursa
mbalimbali ikiwemo hiyo ya amsha kiwanda,ili waweze kufanikiwa kwani yeye
amefanikiwa kutokana na kupatiwa mafunzo na SIDO.
Hata hivyo Mwenyekiti wa TWCC Mwanza Mariam Munanka alisema,
wanatoa elimu kwa wamama
wajasiriamali na kuwawezesha kwenda
kwenye maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kupanua wigo
wa biashara, kuweza kujitambua na
kuzalisha bidhaa bora.
Aidha Katibu wa Jukwaa la Wanawake Mwanza Grace Bunyinyiga
alisema, hiyo ni fursa kwa wanawake mkoani hapa,hivyo wanatakiwa kuunda vikundi
kwa ajili ya kuanzisha viwanda
vidogo,kwani maendeleo ya Mwanza yanaletwa na wao.
Vilevile mmoja wa
washiriki katika kampeni hiyo ambaye ni
mjasiriamali wa kusindika asali
Mariam Nyanza alisema, ni vema mwanamke kujitambua na kufanya kazi ili
kuepuka kuwa tegemezi kwa kuchangamkia
fursa za kiuchumi na biashara zinazotolewa na mashirika mbalimbali.
Mwenyekiti wa TWCC Mwanza, Mariam Munanka akizungumza katika
uzinduzi wa kampeni hiyo.
Meneja
wa SIDO, Bakari Songwe akizungumza katika
uzinduzi
Baadhi ya washiriki wa waliohudhuria uzinduzi huo.
No comments: