Mbunge Ilemela awataka wananchi kuwafichua wauguzi wasio waadilifu
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Judith Ferdinand, BMG
Wananchi wilayani Ilemela wametakiwa kutoa taarifa za
wauguzi wa vituo vya afya vya serikali ambao siyo waadilifu wanaowatoza fedha
za matibabu watoto chini ya umri wa miaka mitano na wazee kuanzia miaka 60.
Wito huo
ulitolewa jana na mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula wakati
akizungumza na wananchi wa Kata ya
Shibula kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Monze.
Dkt.Mabula
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema serikali imeweka utaratibu wa matibabu
kwa watoto chini ya umri wa miaka
mitano, wamama wajawazito na wazee wenye miaka kuanzia 60 kupata huduma za afya
bure katika vituo vyote vya afya vya
serikali hivyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za baadhi ya wauguzi ambao siyo waadilifu na wanaoenda kinyume na taratibu kwa kuwatoza
fedha.
"Kumekuwa
na malalamiko juu ya baadhi ya wauguzi wa afya kuwatoza fedha za matibabu
watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wazee wenye miaka kuanzia 60,
nawaomba mtoe taarifa ili hatua kali
dhidi yao zitachukuliwe huku na nyie
mkitimiza wajibu wenu kwa kupeleka watoto kliniki. Alisema Dkt. Mabula.
Kwa
upande wake diwani wa Kata ya Shibula,
Dede Swila aliwahimiza wananchi kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto
kliniki huku akina mama wajawazito nao wakiwa na utamaduni kwa kuhudhuria
kliniki.
Awali baadhi
ya wananchi wa Kata ya Shibula walitoa malalamiko wa mbunge wao kuhusu baadhi ya wauguzi katika
vituo vya afya kuwatoza fedha pale wanaposhindwa kuhudhuria kliniki kuanzia
muda wa mwezi moja.
No comments: