LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hata kama ni nyumba ya majani peleka umeme- Waziri Kalemani

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani akiongesha kifaa cha UMETA kinachotumika kuunganisha huduma ya umeme kwenye nyumba ambayo haijafungwa waya "Wiring), wakati akizindua huduma ya umeme wa REA III awamu ya kwanza katika Kijiji cha Isangiyo Kata ya Kisesa wilayani Magu, hii leo Julai 24, 2018.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema serikali imedhamiria kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote nchini na kuwataka wananchi kutumia vyema fursa hiyo kuunganishiwa huduma hiyo.

Waziri Kalemani ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua mradi wa umeme vijijini REA III awamu ya kwanza katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambapo amewahimiza wananchi wilayani humo kuhakikisha nyumba zao zinaunganishiwa umeme hata kama hazijaezekwa kwa bati.

"Nimeishawaambia wakandarasi wangu kuwa ni marufuku kuruka nyumba ya mwananzengo iwe ya majani, iwe ya makuti, iwe ya matembe, iwe ya masanva kama anakaa humo peleka umeme”. Amesisitiza Waziri Kalemani.

Aidha amebainisha kwamba mradi wa REA hauna fidia kwa wananchi hivyo wasidai fidia katika maeneo ambayo nguzo zitapita huku akiwahimiza wananchi wenye nyumba ndogo kununua kifaa maalum cha UMETA na kupata huduma ya umeme.

"Kama una nyumba yako ndogo na haijafungwa waya (Wiring) nunueni kifaa cha UMETA kwa mkandarasi na kitawasaidia kupata umeme kwa gharama nafuu". Amesisitiza Mhe.Kalemani wakati akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Isangijo na Bulalu.

Awali akimkaribisha Waziri Kalemani, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amewahimiza wananchi kutoa ushirikiano wa kuwenye utekelezaji wa zoezi la ufungaji umeme kupitia mradi wa REA na ikiwa kuna changamoto serikali itaendelea kuzitatua.

Nao baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Bulalu wilayani Magu wamefurahishwa kufikiwa na huduma ya umeme na kueleza kwamba hatua hiyo itawasaidia kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Mhe.Hilal Elisha (wa pili kulia) baada ya kumkabidhi Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe.Boniventure Kiswaga (wa pili kushoto) kifaa cha UMETA.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza katika Kijiji cha Bulalu wilayani Magu
Mkuu wa Wilaya Magu Mhe.Khadija Nyembo akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza katika Kijiji cha Mahaha wilayani humo
Mbunge Jimbo la Magu Mhe.Boniventure Kiswaga akiwasilisha salamu zake wakati wa uzinduzi wa huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza katika Kijiji cha Bulalu wilayani Magu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Mhe.Hilal Elisha (kushoto) pamoja Mwenyekiti wa CCM wilayani Magu wakifuatilia kwa umakini uzinduzi wa huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza katika vijiji vya Halmashauri ya Magu
Watendaji mbalimbali ambao wako tayari kuhakikisha umeme wa REA III awamu ya kwanza inawafikia wananchi.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza katika Kijiji cha Bulalu wilayani Magu
Wakazi wa Kijiji cha Isangijo wilayani Magu wakifurahia kufikiwa na huduma ya umeme wa REA III awamu ya kwanza
Tazama BMG Online Tv hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.