LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais ahitimisha ziara yake mkoani Songwe

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Imeandaliwa na Songwe RS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku tano Mkoani Songwe mapema leo na kusisitiza ushirikiano baina ya uongozi ili kuharakisha maendeleo.

Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema akiwa ziarani katika wilaya za Momba, Mbozi na Ileje amebaini kuwa Mkoa wa Songwe umebarikiwa kuwa na rasilimali na utajiri mkubwa kinachotakiwa ni viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.

“Nimefurahishwa na kaulimbiu yenu ya maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani na ushirikiano, bila ushirikiano hakuna maendeleo, kauli mbiu hii sasa ionekane kwa vitendo”, amesisitiza.

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na viongozi wote wapende kuwatembelea wananchi kuanzia ngazi za vijiji ili waweze kuwahudumia vizuri na sio kukaa ofisini.

Mhe Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kuzitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana na kubuni miradi mikubwa itayaowaunganisha wajasiriamali wanawake na vijana kutengeneza viwanda ili kuondokana na umasikini.

Amesema mpango wa mkoa wa kuanzisha vituo vya maendeleo vya kata utawezekana na kuwanufaisha wananchi endapo watendapo watajitoa kwa dhati kuufanikisha na mpango huu utaiwezesha Songwe kupaa kiuchumi.

Aidha Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na wale walioko mipakani kuendelea kutunza amani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kufanya ziara mkoani Songwe kuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa atayasimamia yatekelezwe.

No comments:

Powered by Blogger.