LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri Mussa Sima ashitushwa na athari za ukataji miti wilayani Chemba

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Mussa Sima amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya cha Chemba mkoani katika eneo la Farkwa kujionea athari za ukataji miti kwa matumizi ya kuchomea tofali na mkaa.


Mhe.Sima alifanya ziara hiyo jana ambapo alimuagiza Meneja wa Wakala wa Misitu (TFS) mkoani Dodoma kukaa na uongozi wa Wilaya ya Chemba ili kuainisha na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya hifadhi na uvunaji wa misitu na si kuvuna kiholela kama inavyofanyika hivi sasa. 

Pia alitoa rai kwa mikoa mingine nchini kuainisha maeneo ya hifadhi ili yaweze kutangazwa kama maeneo lindwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari za ukataji miti katika eneo la Farkwa Wilayani Chemba. Kushoto ni Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akisisitiza jambo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, mara baada ya kujionea athari za uharibifu wa Mazingira katika eneo la Farkwa. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine. 
Sehemu ya kuni ambazo zinatokana na utakaji wa miti ya asili Wilayani Chemba. Imebainika kuwa kuni hizo hutumika katika uchomaji wa tofali. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ametaka wakazi wa maeneo hayo kutumia pumba ama mashudu ili kunusuru mazingira.
Eneo la msitu  katika wilaya ya Chemba lililoathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za binadamu ikiwemo ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa pia uchomaji wa tofali.
Imeandaliwa na Ofisi ya NWOMRMM

No comments:

Powered by Blogger.