Dkt. Gibai ahamasisha watanzania kutembelea Hifadhi za Taifa
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Watanzania wametakiwa kuendelea kuimarisha utamaduni wa kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii hususani wanyama kupitia utalii wa ndani.
Pia wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Bunda mkoani Mara waliitumia fursa hiyo kutembelea hifadhi ya taifa Serengeti kama ambavyo baadhi yao wanaonekana katika picha akiwemo Katibu wa chama hicho wilaya (wa pili kulia).
"Watanzania tujenge utamaduni wa kutembela hifadhi zetu na kutambua fursa zilizopo kwenye utalii ikiwemo kutengeneza na kuuza bidhaa asilia na kujipatia kipato" alisisitiza Dkt. Gibai.
Tazama picha mbalimbali za wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari kuhusiana na Serengeti
No comments: