LIVE STREAM ADS

Header Ads

Walengwa zaidi ya 3000 waendelea kunufaika na TASAF mkoani Shinyanga

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Manispaa ya Shinyanga, Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.
Na Kadama Malunde, Malunde Blog
Jumla ya walengwa 3,955 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wanaendelea kunufaika na mpango huo katika Manispaa ya Shinyanga.

Hayo yamebainishwa jana Agosti 9,2018 na Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.

Kiwone alisema Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika manispaa ya Shinyanga ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ukiwa na walengwa 4,244 ambao hata hivyo walipungua kutokana na wengine kufariki na wengine tuliwaondoa kwa kukosa sifa za kuwa kwenye mpango lakini mpaka sasa tuna walengwa 3,955.

"Tangu mwaka 2015 mpaka sasa tumepokea fedha za serikali jumla ya shilingi bilioni 3,fedha ambazo tumewapa walengwa ni shilingi bilioni 2.7 na tayari zimewafikia walengwa ambapo fedha hizi zinawasaidia kwa sababu wanapewa fedha kisha kufundishwa namna ya kutumia fedha hizo". Alifafanua.

Alieleza kuwa vipaumbele ni kuhakikisha mlengwa anapata milo mitatu,huduma bora za afya ambapo tunahamasisha wawe na bima za afya, aweze kuhudumia watoto wake na asikose mahitaji madogo madogo na wawe na miradi ya uzalishaji mali kwa sababu serikali haitatoa fedha milele kwa watu wale wale kwani ina wahitaji wengi sana.

"Tunahitaji walengwa waliopo kwenye mpango huu wazitumie hizi fedha zinazotolewa na serikali kujikwamua kimaisha, tunategemea baada ya miaka mitatu tumkute mlengwa akiwa na kitu ambacho kitamfanya aishi,aweze kutoka kwenye hali aliyokuwa nayo kabla ya mpango hu wa kunusuru kaya maskini". Aliongeza Kiwone.

"Kuna walengwa wanafanya vizuri sana,yaani unaona kabisa huyu anachukia kuwa maskini kwa kujitahidi kutumia fedha hizi kujikwamua kimaisha lakini changamoto iliyopo ni baadhi ya watu kutumia vibaya fedha na kushindwa kufikia matarajio yaliyokusudiwa". Alisema.

Hata hivyo aliwaondoa hofu walengwa wa mpango huo wanaodai kuwa serikali imesitisha mpango na kubainisha kuwa bado serikali haijatoa maelekezo yoyote mpaka sasa.

"Huu mradi ni wa miaka 10, kuna watu wanasema mtaani kwamba mradi umeisha,naomba niwaambie kuwa sisi hatujapokea maelekezo yoyote ya serikali mpaka sasa kwamba mradi umeisha na ndiyo maana mwaka huu wa fedha 2018/2019 tumeletewa fedha zingine za kuhawilisha,hivyo pindi tutakapopokea maelekezo ya serikali basi tutawaarifu". Alieleza Kiwone.

Aidha alisema kwa kutambua kuwa afya ni mtaji wa kufikia malengo ya kujikwamua kimaisha asilimia 90 ya wanufaika wa TASAF katika Manispaa ya Shinyanga wamejiunga na mfuko wa bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya kupata huduma bora za afya na kuongeza kuwa wanaendelea kuhamasisha walengwa kujiunga na bima ya afya.

Alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo katika kutekeleza mpango huo kuwa ni walengwa kutumia vibaya fedha zinazotolewa na wengine wanadhani TASAF ni shirika linalotoa misaada kwamba mtu yeyote anaweza kupata ruzuku msaada muda wowote lakini wanaendelea kuwaelimisha kuwa TASAF ni mfuko na una taratibu zake.

Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni walengwa kuhama mtaa bila kufuata utaratibu matokeo yake inafikia wakati pesa za walengwa zinarudishwa makao makuu kwa sababu mhusika anakuwa hayupo kwenye eneo analopaswa kuwepo.

"Walengwa wa Mjini wanaonekana kutofanya vizuri kutokana na kwamba wengi wamepanga kwenye nyumba za watu na wengine wamekuwa wakihama hama na hawana mashamba na maeneo ya ufugaji hivyo tunaendelea kuwahamasisha kufanya ujasiriamali,kufanya biashara ndogo ndogo zinazoendana maeneo na waliyopo". Alisema.

"Walengwa wa Vijijini wanafanya vizuri sana,vitu vinaonekana,mtu atakuonesha kiwanja,mifugo,amesomesha,ameboresha nyumba,Mjini maisha ni gharama kila kitu kinanunuliwa changamoto ni eneo lilivyo maana pesa hiyo hiyo anayopata anailipia pango". Aliongeza Kiwone.

Kwa upande wao walengwa wa mpango huo,licha ya kuipongeza serikali kuwainua kimaisha, waliomba serikali kuongeza fedha kutokana na gharama za maisha kupanda na kwamba mpango huo uwe endelevu.

No comments:

Powered by Blogger.