Maonesho Nane Nane yasiwe nguvu ya soda- Dkt.Mwanjelwa
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri
wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa jana Agosti 04, 2018 amefungua rasmi maonesho
ya kilimo na sherehe za wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi
yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.
“…Maonesho
haya ya Nane Nane ambayo ndiyo ya msingi sana, yasiwe tu kama ni maonesho ya
nguvu ya soda, tunataka tuone matokeo chanya kwa wakulima wetu. Na kwa maana
hiyo ifike mahala basi tuwe na maonesho ya kimataifa…”. Alisisitiza
Dkt.Mwanjelwa.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Mathao Masele alisema yalianza Oktoba
Mosi na yatafikia tamati Agosti 08, 2018 ambapo hadi sasa kuna zaidi ya
washiriki 300 kutoka taasisi na makampuni mbalimbali.
Hii ni mara
ya kwanza maonesho ya Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza,
Geita na Kagera kufanyika baada ya serikali kugawa mikoa ya Kanda ya Ziwa
katika kanda mbili kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Nane Nane. Kanda nyingine
ni Kanda ya Ziwa Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Mhe.Dkt. Severine Lalika akizungumza kwenye maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi, Mathayo Masele akitoa taarifa ya maonesho hayo
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akitoa salamu zake kwenye maonesho hayo
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akijionea kikundi cha ngoma cha Bujora wakati kikitumbuiza kwenye maonesho hayo
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akipokea maelezo kuhusu zao la mpunga kutoka kwa Dkt.Rashid Lussewa (kushoto) ambaye ni mtafiti wa zao hilo Kanda ya Ziwa, Chuo cha Kilimo Ukiriguru
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa alitoa rai kwa wataalam kutoka taasisi ya kilimo Ukiriguru pamoja na Bodi ya Pamba kuhakikisha wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu wa zao la pamba kwani wakulima wengi wamepata hasara kutokana na wadudu hao
No comments: