Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Jijini Mwanza yafana
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Mwenge wa
Uhuru umewasili katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukitokea katika
Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema kwa ajili ya kukagua, kuweka mawe ya
msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenge wa
Uhuru umewasili katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukitokea katika
Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema kwa ajili ya kukagua, kuweka mawe ya
msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Dkt. Philis Nyimbi amepokea Mwenge huo
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole na kubainisha
kwamba miradi itakayopiwa na mbio za Mwenge ina thamani ya shilingi bilioni
4.8.
Mapokezi
hayo yamefanyika mapema leo Agosti 31, 2018 katika eneo la Kamanga Feri ambapo
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho ametumia fursa
hiyo kuwahimiza wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa kuwapa mahitaji muhimu
ya shule watoto wao katika kipindi hiki ambacho serikali inatekeleza mpango wa
elimu bure ili kuwawezesha kupata elimu bora.
Aidha
ameonya kuhusu suala la dawa za kulevya kwa vijana ambapo amewataka kujiepusha
na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa yanahatarisha maendeleo ya taifa na
kuwahimiza kuwa wazalendo.
Baada ya
makabidhiano hayo, Mwenge wa Uhuru umeelekea Kata ya Isamilo na kuweka jiwe la
msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Isamilo-Nyashana-Jeshini inayojengwa kwa
kiwango cha mawe yenye urefu wa kilomita moja kabla ya kuwasili katika eneo la
Soko Kuu katikati ya Jiji la Mwanza ili kukagua shughuli za kiuchumi za vikundi
vya vijana na akinana pamoja na kukabidhi hundi ya shilingi milioni 200 kwa
vikundi 52 vya wajasiriamali vya akina mama na vijana.
Shughuli
nyingine zitakazofanywa na Mwenge ni pamoja na uzinduzi wa mradi wa mfumo
rahisi wa maji taka katika maeneo ya miinuko uliopo Kata ya Igogo, kutembelea
soko la kisasa la Igogo, kukagua duka la kisasa la usambazaji wa pembejeo za
kilimo la Twiga Chemical Industrial lililopo Kata ya Mkuyuni, kuweka jiwe la
msingi kwenye mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya wilaya Nyamagana
iliyopo Butimba.
Pia mwenge
utazindua Klabu ya kupambana na rushwa katika shule ya msingi Nyakato B,
kufungua Zahanati ya Isebanda Kata ya Lwanhima, kukagua shughuli za udhubiti
ugonjwa wa Malaria Kata ya Lwanhima, kugawa kadi za kupata matibabu kwa wazee
Kata ya Lwanhima na kukagua zoezi la upimaji Saratani ya shingo ya matiti Kata
ya Lwanhima na kufungua shule ya msingi Buhongwa B Kata ya Buhongwa.
Baada ya
shughuli hizo, Mwenge wa Uhuru utaelekea eneo la mkesha katika eneo la shule ya
msingi Buhongwa B ambapo utafanyika ukaguzi wa mabanda ya maonesho ya bidhaa na
huduma mbalimbali, kusoma risala ya utii ambapo kesho Septemba Mosi, 2018 utakabidhiwa
katika wilaya ya Ilemela ambapo makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja
vya Mwatex.
Mwenge wa Uhuru wakagua miradi kabambe Misungwi
Tazama BMG Online Tv hapo chini
Mwenge wa Uhuru wakagua miradi kabambe Misungwi
No comments: