Masanja atamba kufanya kweli Jijini Mwanza
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Mchekeshaji
na mwimbaji wa nyimbo za njili hapa nchini, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja
Mkandamizaji amewataka wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kujitokeza kwa
wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa albamu ya “Tuliza Mawimbi” iliyoandaliwa na
kwaya ya Ebenezer Family Band.
Amesema
katika uzinduzi huo utakaofanyika leo September 09, 2018 katika uwanja wa CCM
Kirumba, atatumbuiza nyimbo zake mbalimbali ikiwemo wimbo wake mpya uitwao
Kemea Pepo.
“Naomba
wakazi wa Mwanza wafike bila kukosa iwe kwa usafiri wa gari, baiskeli, bajaji
hata kwa miguu ili washuhudie uzinduzi huo na kumsifu Mungu kupitia injili”.
Amesema Masanja.
Uzinduzi huo
pia utahudhuriwa na kwaya mbalimbali ikiwemo AIC Makongoro, Revival Mission
Band na Emaus Band ambapo kiingilio ni shilingi 2,000 kwa watu wazima na shilingi
elfu 1,000 kwa watoto.
No comments: