LIVE STREAM ADS

Header Ads

Profesa Kikula aongoza kikao kazi Tume ya Madini

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.


Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.

Na Greyson Mwase, Tume ya Madini

Jna Septemba 25, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliongoza kikao kazi cha tume hiyo Jijini Dodoma kilicholenga kujadili utendaji kazi wake katika kipindi cha robo mwaka (Julai hadi Septemba).

Kikao hicho kilishirikisha pia viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Profesa Shukrani Manya, Makamishna wa Tume Dkt. Athanas Macheyeki, Profesa Abdulkarim Mruma,  Haroun Kinega, Dkt. Florens Tunuka, Dkt. Evaristo Longopa pamoja na watendaji wengine kutoka Tume.

Kati ya masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupata taarifa za utendaji za kamati za Tume ya Madini katika kipindi cha robo mwaka na namna ya uboreshaji wa huduma za leseni.

No comments:

Powered by Blogger.