"Sehemu pekee ya vijana kuimarisha kipato ni sekta ya Kilimo"- Dkt Tizeba
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Dkt Charles
Tizeba Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi
maalumu ya kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza
Dkt Charles
Tizeba Waziri wa kilimo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela
wakikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza wakati walipotembelea kambi
maalumu ya vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa
Tanga walioamua kufanya ujenzi kwa kujitolea, wakati akiwa safarini kuelekea
Wilayani Korogwe
Waziri wa
kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na
vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao
wapo katika kambi maalumu wakijitolea katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya
Muheza.
Na Mathias Canal-WK, Muheza-Tanga
Imeelezwa
kuwa sehemu pekee ya kuimarisha kilimo cha mwananchi mmoja mmoja, wananchi
katika makundi ya kijamii hususani vijana ni kupitia sekta ya kilimo kwani ndio
sehemu pekee ya ukombozi wa mkulima katika jamii.
Imeelezwa
kuwa kuna uwezekano wa kufanya biashara mbalimbali nchini ambazo zinaweza
kuongeza kipato lakini sahemu sahihi isiyokuwa na jazba na dhoruba katika
utendaji ni kufanya kilimo biashara ambacho kamwe hakiwezi kumtupa mkulima.
Dkt Charles
Tizeba Waziri wa kilimo, ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba 2018 wakati
akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa
Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya
Muheza.
Vijana hao
ambao wameamua kutumia nguvu zao pasina malipo wameamua kwa umoja wao kuunga
mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli yake inayohamasisha
chachu na juhudi za kiutendaji kwa wananchi ya "Hapa Kazi Tu".
Aidha,
katika kuhamasisha juhudi za kiutendaji Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo
ameunga mkono juhudi za vijana hao kwa kuchangia fedha ya chakula shilingi
1,100,000 sambamba na kushiriki ujenzi wa jengo maalumu la upasuaji.
Waziri wa
kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alitembelea ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya
Muheza akiwa safarini kutembelea mashamba ya mkonge ikiwa ni siku ya pili ya
ziara ya kikazi Mkoani Tanga aliyoianza jana tarehe 25 Septemba 2018 ya
kukutana na makundi mbalimbali ya wakulima wa zao la Mkonge ili kutafuta
ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo.
No comments: