LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mamia wahudhuria mazishi ya waliofariki ajali ya kivuko cha MV. Nyerere

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia waombolezaji mbalimbali waliohudhuria mazishi ya abiria aliofariki katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. 

Majaliwa aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi hayo yaliyofanyika jana Septemba 23, 2018. Ajali ya kivuko hicho kilichokuwa kikifanya safari zake kati ya visiwa vya Bugorola na Ukara wilayani Ukerewe ilitokea Septemba 20, 2018.
Baadhi ya waombolezaji
Baadhi ya waombolezaji
Viongozi mbalimbali waliohudhuria mazidhi hayo
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa kwenye mazishi hayo
Zoezi la kuhifadhi miili tisa iliyozikwa katika makabuli ya pamoja
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye makaburi hayo
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya UVCCM na UWT Taifa Wakitoa heshima zao
Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza wakitoa heshima
Viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na wananchi wameshiriki mazishi ya pamoja ya abiria waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV. Nyerere yaliyofanyika jana Septemba 23, 2018 wilayani Ukerewe. Ajali ya kivuko hicho kilichokuwa kikifanya safari zake kati ya visiwa vya Bugorola na Ukara wilayani Ukerewe ilitokea Septemba 20, 2018.
Picha na Fahadi Siraj, UVCCM

No comments:

Powered by Blogger.