LIVE STREAM ADS

Header Ads

Washindi UMITASHUMTA 2018 wilayani Misungwi wapongezwa

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza limewapongeza wachezaji walioshiriki mashindano ya umoja wa michezo, sanaa na taaluma kwa shule za msingi UMITASHUMTA 2018 baada ya kuibuka na ushindi.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Antony Bahebe ametoa pongezi hizo leo kwenye mkutano wa robo ya nne ya mwaka 2017/18, uliolenga kujadili taarifa za maendeleo za mwaka.

Kupitia kikao hicho, Baraza hilo limepokea rasmi makombe 14 ya ushindi yaliyotokana na ushindi huo na kuahidi kuandaa zawadi maalum kwa ajili ya wachezaji hao ambapo itakabidhiwa hivi karibuni.

Afisa Michezo Wilaya Misungwi, Mwl. Sixbert Mbwambo amesema katika mashindano hayo yaliyofanyika Mei 31 hadi June 03 mwaka huu katika kituo cha shule ya sekondari ya wavulana Bwiru, wilaya hiyo iliibuka mshindi wa kwanza kwa mkoa Mwanza na kujinyakulia vikombe 14 kati ya 21.

Mwl. Mbwambo amesema wilaya Misungwi ilitoa wanafunzi 34 kati ya 120 ili kutengeneza timu ya mkoa Mwanza iliyoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA kitaifa ambapo Mwanza iliibuka mshindi wa kwanza.

Wachezaji waliopongezwa wanaunda wa timu za michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete,mikono, wavu na riadha ambapo wametoa pongezi kwa baraza hilo na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.


Pia itakumbukwa kwamba Halmashauri ya Misungwi iliibuka nafasi ya nne kati ya Halmashauri nane mkoani Mwanza kwenye mashindano ya umoja wa michezo, sanaa na taaluma kwa shule za sekondari UMISSETA 2018 yaliyofanyika kituo cha shule ya sekondari Nsumba huku mkoa Mwanza ukiibuka nafasi ya pili kitaifa.
Mwenyekiti Halmashauri ya Mwisungwi, Antony Bahebe (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri hiyo Mwl. Kisena Mabuba (kulia) wakiwa na kombe la ushindi mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Misungwi, Daud Gambadu (kushoto), pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Juma Sweda (kulia) wakiwa na kombe la ushindi mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Misungwi, Daud Gambadu (kulia), pamoja na Katibu wa CCM wilayani Misungwi Latifa Malimi (kushoto) wakiwa na kombe la ushindi mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Misungwi, Mwl Kisena Mabuba akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo
Afisa Elimu Msingi wilayani Misungwi, Mwl. Ephraim Majinge akifurahia ushindi wa wanafunzi wake
Wachezaji wa UMITASHUMTA 2018 wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Tazama BMG Online Tv hapa chini

SOMA Halmashauri ya Misungwi yaibuka bingwa mashindano ya UMITASHUMTA

No comments:

Powered by Blogger.