LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tamasha la Urithi lazinduliwa Jijini Dar es salaam

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi jijini Dar es Salaam, kushoto ni Profesa Audax Mabula ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Tanzania.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi. Devotha Mdachi akitoa neno la shukurani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi Jijini Dar es Salaam.
 Bi. Perpetua Ishika (kushoto) akitoa maelezo mbalimbali kuhusiana na Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania na kuwasihi watanzania kuchukua fursa na kujiunga katika chuo hicho. Kulia aliye vaa suti nyeusi ni mgeni rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania.
 Afisa Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania Bw. William Haule (kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na kazi mbalimbali wanazozifanya kuhusiana na maswala ya utalii pamoja na maelezo mafupi yaliyohusu maonesho makubwa ya Swahili International Tourism  Expo (SITE) yatakaloanza tarehe 12  hadi 14 Oktoba 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar.
Bi. Monica Mutoni ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (Kushoto aliyeshika kinasa sauti) akitoa maelezo mbalimbali kuhusu uhusiano baina ya hali ya hewa na utalii, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wachoraji aliyefika katika Tamasha la Urithi Bw. Vicent Temu akitoa maelezo kuhusiana na kazi yake ya uchoraji wakati mgeni rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wadau wa utalii Tanzania alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali.
Hii ni moja ya picha ambayo imechorwa na Bw. Vicent Temu ambayo ametumia penseli pekee.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi akitazama na kupata maelezo katika moja ya picha iliyochorwa na Vicent Temu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Roots and Shoots wakitoa maelekezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na kazi mbalimbali za sanaa wanazozifanya kwa kutumia vitu mbalimbali iliwemo na maboksi, mbao, shanga, ngozi na vitu mbalimbali.
Bi. Deborah Mjata ambaye ni mbunifu kwa njia ya kuchonga(aliyeshika kinasa sauti) akimpa maelezo mgeni rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wadau wa utalii Tanzania (aliyevaa Suti nyeusi) alipotembelea banda hilo.
Bi. Debora Mjata ambaye ni Afisa Masoko wa Rike Enterprises (katikati) akitoa zawadi ya sanamu aliyoichonga yeye mwenyewe kwa niamba ya kampuni yao ya Rike Enterprises kwa mgeni rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wadau wa utalii Tanzania (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi Devotha Mdachi.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi. Devotha Mdachi (wa pili kutoka kulia) akitazama kazi mbalimbali za wabunifu kwa kutumia batiki.
 Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania (aliyevaa suti nyeusi) akitazama ubunifu wa moja ya wadau wa sanaa anayefinyanga vitu mbalimbali kwa kutumia udongo na unga wa mbao.
Vijana wanaotengeneza vitu vyao kwa kutumia ngozi.
kulikuwa na ofa maalum ya kula nyama ya Nyumbu
Uzinduzi wa Tamasha la Urithi ulifanyika jana Oktoba Mosi, 2018 Jijini Dar es salaam ikiwa ni mkoa wa pili baada ya kuzinduliwa kitaifa na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Picha na Fredy Njeje

No comments:

Powered by Blogger.