LIVE STREAM ADS

Header Ads

TARIME: Serikali yatakiwa kuchukua hatua kali kwa wanaokeketa watoto wa kike

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Eliafile  Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika Kijiji cha Pemba na Kyoruba Juu kuhusu madhara ya ukeketaji.
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza mwezeshaji.
Christina Edward ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyabisaga Kata ya Pemba akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Ghati Samweli ambaye ni mwezeshaji kutoka shirikala Tanzania Mindset Network akitoa elimu ya kupinga ukeketaji katika Kijiji cha Nyabisaga wilayani Tarime.
Picha ya pamoja baina ya wakufunzi na washiriki wa mafunzo ya kupinga ukeketaji wilayani Tarime.
Eliafile  Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu juu ya madhara ya Ukeketaji  kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika Kijiji cha Pemba na Kyoruba wilayani Tarime.
Mzee Rouben Makuri ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyoruba akichangia mada kuhusu kupinga ukeketaji kwa mtoto wa kike. 

Na Frankius Cleophace Tarime
Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali kwa wazazi na walezi wilayani Tarime ambao wanakubali kukeketa watoto wa kike ambao hukimbia ukeketaji  kipindi hicho na baada ya zoezi kumalizika mabinti hao waliokimbia hukamatwa na kukeketwa.

Hivyo serikali imehimizwa kuendelea kusimamia vikali sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ili kutokomeza suala la ukeketaji kwa mtoto wa kike huku baadhi yao wakikeketwa usiku.

Hayo yamebainisha na baadhi ya wazazi katika Kata ya Pemba wakati wakipatiwa elimu ya kupinga ukeketaji kupitia shirika la Tanzania Mindset Network chini ya ufadhili wa TGNP Mtandao kupitia shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA.

Wazazi hao wamedai kuwa kipindi cha ukeketaji watoto wamekuwakikimbia ili wasikeketwa mpaka msimu wa ukeketaji unamalizika lakini pale wanarudi kijijijini ukamatwa na jamii na kukeketwa kwa Nguvu hivyo wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaoshiriki katika kitendo hicho.

”Kuna ngariba tunamfaamu yuko maeneo ya mbali ameibuka hivi karibuni tunajua atakeketa watoto wetu usiku hivyo serikali itambue suala hilo” alisema mmoja wa wazazi katika Kijiji cha Nyabisaga.

Thomas Muruga ambaye ni Mratibu wa Shirila la Tanzania Mindset Network anasema kwa sasa wameamua kutoa elimu ya kupinga ukeketaji kwa kutembelea nyumba kwa nyumba huku wakifanya mikutano ya hadhara katika Kata 13 wilayani Tarime ili kutoa elimu hiyo kwa lengo la kuwanusuru watoto wa kike wasikeketwe.

Pia Muruga amesema nia ya shirika hilo ni kuwafikia wazazi, walezi, watoto wa kike, Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji ili kutoa elimu hiyo nao waweze kuwa mabalozi kwa lengo la kupinga Ukeketaji.

Mwita Chacha ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabisaga akizungumzia suala la watoto wa kike kukeketwa nNyakati za usiku, alisema bado taarifa hizo kama viongozi hawajapelekewa lakini tayari wamepiga marufuku suala la ukeketaji na kuhaidi kuchukua hatua kali kwa mzazi au mlezi atakayeshiriki kwa aina yeyote kukeketa mtoto wa kike.

Naye Rhobi Kemahi ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongozji cha Nyaibara alishauri elimu kuendelea kutolewa kuanzia  kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji na Kata ili kusimamia vikali suala hilo pamoja na kufikisha elimu hiyo maeneo ya pembezoni na siyo mjini tu. 


Aidha  Eliafile Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la Tanzania Mindset Network amesema wazazi na walezi wakipata elimu hiyo itasaidia sana kwani wao ndio wanaishi na watoto hivyo amewaomba wazazi hao kuacha kupeleka watoto wao ili kukeketwa.
SOMA>>>TARIME: Wazee wa Kimila, Mangariba waonya kuhusu Ukeketaji

No comments:

Powered by Blogger.