Umoja wa Makondakta Mwanza wagawa sare kwa wanachama wake
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Judith Ferdinand, BMG
Katika
kuhakikisha wanaondoa vitendo vya kihalifu ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya,
lugha za matusi na wizi katika maeneo ya stendi, makondakta na wasaidizi
wao (wapiga debe) wa daladala mkoani Mwanza wameanzisha umoja wao.
Akizungumza
katika kikao maalumu kwa ajili ya kuwagawia sare wanachama wa umoja huo, Mwenyekiti wa umoja
wa Makondakta na wasaidizi wao (UVDS) Mkoa wa Mwanza, Mrimi Juma alisema lengo la kuanzisha umoja
huo ni kutatua kero zinazotokea katika maeneo ya stendi pamoja na kubadili
mtazamo wa abiria na jamii ambayo imekuwa ikiwachukulia kama walevi, wezi na
kuwa ni vijana wasio jitambua sanjari na kusaidizana katika masuala mbalimbali.
Juma
alisema kupitia umoja huo ambao mpaka sasa unajumla ya wanachama 500, watakuwa
na sare ambazo zina namba pembeni, zitakazosaidia kuwatambua kama ni wanachama
na endapo watafanya uhalifu itakuwa ni rahisi kuwagundua kwani kupitia namba
hizo tutamjua muhusika kwani kuna baadhi wanafanya uhalifu alfu wanasingiziwa
wapiga debe.
Aliahidi kuwa Disemba mwaka huu kila wanachama atakatiwa bima ya afya ambayo itawasaidia katika kupata
matibabu ambayo yanagharama kubwa licha ya kuchangishana fedha pale mwenzao
anapokuwa amepata matatizo ila hazitoshi ukilinganisha na kipato chao,na
kuanzia januari hadi februari mwakani watawapeleka chuo cha Veta ili waweze kupata leseni.
Kwa upande
wake Polisi Kata wa Kata ya Buhongwa, Afande Juma Salum ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika kikao hicho aliwataka makondakta
na wasaidizi wao kuipenda kazi yao kwa kuwa wasafi na kuacha lugha za matusi
kwani kazi hiyo ni kama nyingine na wahakikishe wanafuata na kutekeleza yale
waliokubaliana yeye atayasimami na kwenye kazi hana urafiki na mtu anacho
angalia ni sheria.
Suala la
sare kwa wanachama wa umoja huo ni zuri kwani litawasaidia kujua nani siyo
mwenzao, pia wawe na utaratibu wa kuhakikisha kila asubuhi wanaripoti na
kusaini kwa viongozi wa umoja huo katika vituo vyao vya kufanyia kazi, kwani jicho
la wengi lilikua likiwaangalia tofauti na kuwaona ni wahuni.
Naye Katibu
wa umoja huo, Erick Felician alisema lengo la umoja huo ni kusaidiana katika
shida na raha ikiwemo kukopeshana mikopo ambayo haina riba ili waweze
kukikomboa kiuchumi kwa kuanzisha shughuli za ujasiriamali pamoja na kuanzisha
timu inayotokana na umoja huo kwani wanaamini michezo ni ajira na huleta watu
pamoja.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Makondakta mkoani Mwanza (UVDS), Mrimi Juma akizungumza katika kikao na
wanachama wake kilichofanyika jumapili iliyopita katika ofisi za umoja huo Buhongwa Jijini Mwanza.
No comments: