“Umuhimu wa mbolea ni pale inapomfikia mkulima shambani sio kuwa ghalani”- Dkt. Tibeza
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza na wanachama wa chama cha Tuungane wakulima Interpises katika kijiji cha Mbugani kilichopo kata ya Itunundu Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini, jana Oktoba 12, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua
mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa kwa
ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mpunga katika ziara ya kikazi ya kukagua
hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashamba ya mpunga alipotembelea Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua Ghala la kuhifadhi mpunga la Tuungane Wakulima Inteprises wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Iringa.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashine ya kukoboa mpunga ya Chama cha Tuungane Wakulima Inteprises.
Na Mathias Canal-WK, Iringa
Serikali imesema
itahakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati kabla ya kuanza msimu wa
kilimo wa mwaka 2018/19 kwani umuhimu wa mbolea ni pale inapowafikia wakulima
shambani sio kuhifadhiwa ghalani.
Katika msimu
ujao Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea na pembejeo
nyingine katika maeneo yao wakati wote wanapohitaji ili kuondoa adha ya muda
mrefu ya mbolea kuchelewa kuwafikia wakulima kwa wakati.
Waziri wa
Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na
wanachama wa chama cha Tuungane wakulima Interpises akiwa katika ziara ya
kikazi kata ya Itunundu Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea
katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Dkt. Tizeba
amesema kuwa ili kuboresha usambazaji wa pembejeo kwa wakulima katika msimu wa
mwaka 2017/2018 mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-
BPS) umeongeza upatikanaji wa mbolea kwa wingi, bei nafuu na wakati.
Aidha, kwa
kutumia utaratibu huo bei za mbolea aina ya DAP na UREA zimepungua kwa wastani
wa asilimia 30.
Akifafanua
zaidi, Dkt Tizeba alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) inaendelea
kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na pindi ukiukwaji wa bei elekezi unapobainika
hatua stahiki zinachukuliwa kwa wahusika.
”Endapo kama
kuna mtu atapandisha gharama za mbolea kwa kupandisha bei maradufu zaidi ya bei
elekezi serikali itamchukulia hatua haraka za kisheria atakayebainika ”
Alikaririwa Dkt Tizeba
Katika
kuimarisha sekta ya kilimo serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali
kuimarisha kilimo kwa kuwekeza katika pembejeo, mbolea na zana zinazoweza
kuikuza sekta ya kilimo ili iweze kuchochea uchumi wa viwanda.
Kadhalika,
Waziri Tizeba amewatoa hofu wakulima nchini kuwa kuna akiba ya mboleaya awali
isiyopungua Tani 80,000 kwa ajili ya kupandia.
No comments: