LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM mkoani Geita yaahidi kusimamia vyema fedha za miradi ya kijamii

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Na Edwin Soko, Geita
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita kimeahidi kuisimamia kikamilifu Serikali ya Mkoa kwenye utekelezaji wa miradi ya huduma za kijamii na kuhakikisha wakanzi wa Geita wananufaika na huduma za kijamii kwa kuboresha maisha yao.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi alipokuwa anaongea na mwandishi wa habari hii.

Kidushi alisema kuwa, ana wajibu wa kuisimamia Serikali Mkoani humo katika kuhakikisha inatekeleza vyema wajibu wa kusimamia vyema fedha za miradi ya kijamii inayofadhiliwa na kampuni ya Geita Gold Mine, inayojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu Mkoani humo.

“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali ya utekelezaji na moja ya mikakati yake ni kuona wananchi wanaoishi kwenye maeneno ya migodini wananufaika kupitia uwekezaji unaofanywa kwenye maeneno yao, hivyo ni wajibu wangu kuisimamia Serikali ya Mkoa na kuhakikisha awamu hii ya tano hakuna ufujaji wa pesa zinazotengwa kwa ajili ya huduma za miradi ya kijamii” Alisema Kidushi.

Hellena Maduhu mkazi wa Mkoa wa Geita, alisema kuwa, Serikali ya awamu ya tano imesimamia vyema utekelezaji wa usimamizi wa miradi ya kijamii na miradi mingi sasa inatekelezwa vyema Mkoani humo, ikiwemo ujenzi wa mnara wa saa, uwekeji wa taa za barabarani, ujenzi wa shule ya Sekondari ya mchepuo wa kiingereza ya Buhalahala, ujenzi wa Zahanati za Nyakahongola, Nyarembo na Ikurwa.

Machi 8 mwaka huu, kampuni ya Geita Gold Mine iliingia mkataba na Halmashauri za Geita kutekeleza miradi ya huduma za kijamii katika maeneo ya elimu, afya, usambazaji wa maji, misaada ya kibinadamu na kuendeleza biashara ndogondogo.

Msimamizi wa miradi ya kijamii kutoka kampuni ya GGM, Moses Rusasu alisema kuwa kampuni hiyo iliweka kusudio la kutumia shilingi bilioni 9.124 ambapo shillingi billioni moja itatumika kwenye miradi iliyopo katika Halmashauri ya Geita mjini na shillingi bilioni 1.3 zitatuka kwenye Halmashauri za Bukombe, Chato na Mbongwe.

Utekelezaji wa miradi ya huduma za jamii sasa upo kisheria baada ya marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017 na marekebisho yake ya mwaka 2017 kifungu cha 105 sehemu ndogo ya 1 na 2 inayoainisha wajibu wa kisheria kwa kampuni za uchimbaji wa madini kuwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa fedha za miradi ya kijamii (CSR) na mpango huo lazima upitishwe na mkutano mkuu wa Kijiji, Serikali za Mitaa kwa ushauri wa Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI).

No comments:

Powered by Blogger.