LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Biteko achangia miradi ya maendeo jimboni Bukombe

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.

Akizunguma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03, 2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Shilabela pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Nyamagwangala.

Biteko alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.