LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkutano wa Afrika wa Usimamizi wa Mtandao wafanyika Sudan

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Matangazo.

Edwin Soko- Khartoum, Sudan
Mkutano wa mkubwa wa usimamizi wa mtandao Afrika unaendelea kwa washiriki kutakiwa kutoka na majinu ya changamoto zinazolikabili bara la Afrika na kujua nini cha kufanya kwenye kutumia uchumi wa kijitali kwa teknolojia inayochipukia Afrika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia Nchini Sudan Bwana Bushara Gumaa alipokuwa anafungua rasmi mkutano huo wa siku tatu, Bwana Gumaa alisema kuwa kuikwepa teknolojia haiwezekani katika karne hii, cha msingi ni kuhakikisha Umoja wa Nchi za Afrika (AU) unaweka sera na miongozi mizuri na kuwataka wanachama wa umoja huo kuzitekeleza ili kusukuma mbele jitihada za kila raia kufikiwa na mtandao na kuutumia kwa ajili ya kukuza uchumi wa Afrika.

Pia amesema kuwa , wao kama wenyeji wa mkutano huo kwa mwaka huu wanajisikia faraja sana kupata nafasi hii na watahakikisha wanafanya kazi na Umoja wa Nchi za Afrika bega kwa bega .

Pi katibu mkuu wa wa IGF bwana Makane Faye alizungumza kuwa, mkutano huu wa internet una umuhimu mkubwa kwa bara la Afrika, kwa kuwa matumizi ya mtandao duniani yamekuwa makubwa na hii itasaidia kuona wapi tumefanya vizuri na wapi bado pana changamoto ili kuja na mikakati ya kutatua..

Takwimu zilizowasilishwa na shirika la UNESCO katika mkutano huo zinaonyesha kuwa, ni asilimia 54 tu ya wakazi wa Afrika ndio waliounganishwa na huduma za kimtandao, hivyo jitihada za kipekee zinahitajika kwenye kuhakikisha watu wengi wanapata huduma za mtandao Afrika

Katika mkutano huo Tanzania pia ilipata nafasi ya kushiriki na pia kuwa miongoni kwa sekretarieti ya mkutano wa IGF.

Mkutano huu ufanyika kila mwaka ambapo wadau toka serikarini, wafanyabishara, azaki na wananchi wa kawaida hupata nafasi ya kuhudhuria.

No comments:

Powered by Blogger.