LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Mwanza alamba Nondo ya Uzamivu

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Matangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza, Danford Muyango (pichani) ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dodoma “UDOM” na hivyo kuwa daktari mpya kwa sasa anayefanya kazi na benki hiyo.

Sasa atafahamika kama “Dkt. Danford Muyango” akiwa ni miongoni mwa vijana wachache nchini waliofikia hatua hiyo kielimu. Dkt. Muyango amehitimu Ndaki ya Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii akibobea kwenye fani ya taasisi ndogondogo za fedha na maendeleo ya wanawake.

Dkt. Muyango alitunukiwa shahada hiyo Novemba 23, 2018 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM ambaye pia ni Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mhe. Benjamin Willium Mkapa.

“Namshukru Mwenyezi Mungu pamoja na wale wote waliotoa mchango wao wa hali na mali kuhakikisha nafikia hatua hii, hivyo ni wajibu wangu sasa kuendelea kuitumikia jamii kwa ari kubwa”. Alisema Dkt. Muyango.
Dkt. Danford Muyango (kushoto), akitunukiwa Digrii ya tatu ya Uzamivu (PhD), na Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM Mhe. Benjamin Mkapa kwenye mahafali ya tisa ya chuo hicho yaliyofanyika Novemba 23, 2018. Dkt. Muyango amehitimu Ndaki ya Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii akibobea kwenye fani ya taasisi ndogondogo za fedha na maendeleo ya wanawake.
Dkt. Danford Muyango akiwa kwenye mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu cha UDOM yaliyofanyika Novemba 23, 2018 Jijini Dodoma.
Dkt. Danford Muyango (kushot), akiwa na Msimamizi "Supervisor" wake wa PhD, Dkt. Rehema Kilonzo (kulia).
Dkt. Danford Muyango (kulia) akiwa pamoja na baba yake mzazi, Mzee Muyango.
Dkt. Danford Muyango akiwa pamoja na wanafamilia.
Dkt. Danford Muyango akiwa na mkewe Neema Muyango pamoja na watoto wake Davina na Delvin
Dkt. Muyango amehitimu Ndaki ya Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii akibobea kwenye fani ya taasisi ndogondogo za fedha na maendeleo ya wanawake.
Dkt. Danford Muyango (kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM, Utafiti, Taaluma na Ushauri Profesa Msofe (kulia).
Dkt. Danford Muyango (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.

No comments:

Powered by Blogger.