Zaidi ya wanafunzi 4,000 hatarini kukosa masomo wilayani Ilemela
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Zaidi ya
wanafunzi 4,000 waliohitimu darasa la saba mwaka huu na kufaulu, wako hatarini
kukosa fursa ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani kutokana na upungufu
wa vyumba vya madarasa katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyasema hayo jana wakati akipokea mifuko 100 ya
saruji kutoka benki ya Diamond Trust (DTB).
Dkt. Mabula
alisema wanafunzi 8,350 wamefaulu mtihani wao wa darasa la saba lakini kuna upungufu
wa vyumba 84 vya madarasa hivyo wenye uhakika wa kujiunga na elimu ya kidato
cha kwanza ni wanafunzi takribani 4080. Wilaya ya Ilemela ilishika nafasi ya
kwanza kwa ufaulu mkoani Mwanza na kitaifa nafasi ya sita.
Hivyo Dkt.
Mabula alisema mifuko hiyo ya saruji kupitia taasisi yake ya The Angeline
Foundation inayoshirikiana vyema na Halmashauri ya Ilemela, itasaidia kufyatua matofali
kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu
wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza ambapo aliwahimiza
wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.
Naye Meneja
wa DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor alisema benki hiyo itaendelea kuwa
mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii katika
Mkoa Mwanza hususani katika sekta ya elimu na afya.
Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu, Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor, Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita.
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula akishiriki zoezi la kupanda miti iliyotolewa na Benki ya "DTB" katika Shule ya Msingi Kitangiri C
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu (kushoto), Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor ( wa pili kulia) na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: