LIVE STREAM ADS

Header Ads

Profesa Kikula aongoza kikao kazi cha Tume ya Madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kamishna kutoka Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma (kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha Tume ya Madini kilichofanyika Desemba 21, 2018 jijini Dodoma. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
Kutoka kushoto makamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega na Dkt. Athanas Macheyeki wakifuatilia majadiliano mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea katika kikao hicho.
Kutoka kushoto mbele makamishna wa Tume ya Madini ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florence Turuka wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (hayupo pichani).
Sehemu ya wajumbe kutoka Tume ya Madini wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yanaendelea katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Dkt. Abdulrahaman Mwanga akieleza jambo katika kikao hicho.
Sekretarieti kutoka Tume ya Madini ikinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA kutoka Tume ya Madini, Terence Ngole (katikati) akielezea mikakati ya Tume kwenye utoaji wa leseni kwenye kikao hicho. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Julius Moshi na kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Dkt. Abdulrahaman Mwanga.

Na Greyson Mwanza, Wizara ya Madini
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo ameongoza kikao kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika Jijini Dodoma. 

Kikao hicho kimewashirikisha Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Nchini (FEMATA), Haroun Kinega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Tume na Mpango Mkakati wa Tume wa miaka mitano (2019/20 -2023/2024). 

Katika kikao hicho, kati ya masuala yaliyokubaliwa ni pamoja na leseni za wachimbaji madini ambazo hazifanyiwi kazi kufutwa na tathmini ya kina kufanyika kwa waombaji wa leseni ili kubaini kama wanakidhi vigezo ikiwemo uwezo wa kifedha na utaalam.

No comments:

Powered by Blogger.