LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mama amshukru Rais Magufuli, amwongeza miaka 15

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Mama Madina Mbunda ambaye ni mkazi wa Katunguru wilayani Sengerema ametoa pongezi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyoendelea kuboresha sekta ya afya ikiwemo ukarabati wa Vituo vya Kituo Afya kama vile Katunguru na kutaka aendelee kuwa Rais hata baada ya muda wake kumalizika.

Mama Mbunda alitoa kauli hiyo jana baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kufanya ziara katika Kituo cha Afya Katunguri kilichopewa shilingi Milioni 400 na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano mapya ambayo ni nyumba ya mtumishi, maabara, wadi ya wazazi, jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifahia maiti kupitia mfumo wa “Force Account”.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.