Mkuu wa Mkoa Mwanza afuta mapumziko ya Krismasi na Mwaka Mpya
Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella amefuta mapumziko ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya
2019 kwa watumishi wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, baada ya ujenzi
na ukarabati wa Kituo cha Afya Kome kutokamilika kwa wakati.
Mongella
alitoa agizo hilo jana baada ya kufanya ziara katika Halmashauri ya Buchosa na
kuagiza hadi kufikia Januari 10, 2019 atakaporudi katika Kituo cha Afya Kome akute
ujenzi na ukarabati wake umekamilika.
Serikali
ilitoa shilingi milioni 400 katika Kituo cha Afya Kome kwa ajili ya ukarabati
na ujenzi wa majengo matano mapya ambayo ni nyumba ya mtumishi, maabara, wadi
ya wazazi, jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifahia maiti kupitia mfumo
wa “Force Account”.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akipokelewa na viongozi wa CCM na Serikali baada ya kuwasili katika Kituo cha Afya Kome, Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), akiwa ameambatana na Mkurugenzi Halmashauri ya Buchosa, Chrispin Luanda (kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikagua ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Kome.
Miongoni mwa majengo mapya katika Kituo cha Afya Kome.
Jengo la chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kome.
Nyumba ya mtumishi katika Kituo cha Afya Kome.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati), akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: