KaziNzuri: Mongella aagiza Mhandisi apandishwe cheo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati na
ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakaliro kilichopo Halmashauri ya Buchosa wilayani
Sengerema na kuridhishwa na kasi iliyopo.
Kutokana na
kasi hiyo, Mongella amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa,
Chrispin Luanda kumwandikia barua ya kumpandisha cheo Mhandisi anayesimamia
ujenzi huo, Rahim Mgimba kuwa Kaimu Mkandarasi wa Halmashauri hiyo.
Mongella
alitoa kauli hiyo jana Disemba 18, 2018 baada ya kufanya ziara katika Kituo
hicho kilichopewa shilingi Milioni 400 na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
ya mtumishi, maabara, wadi ya wazazi, jengo la upasuaji pamoja na jengo la
kuhifahia maiti kupitia mfumo wa “Force Account”.
Ujenzi wa majengo mbalimbali katika Kituo cha Afya Nyakaliro wilayani Sengerema.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: