Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua miradi ya maendeleo usiku
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Jana Disemba 18,
2018 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi
wa Hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, yenye hadhi ya
Wilaya inayojengwa katika eneo la Isaka.
Mongella
aliyekuwa na ziara ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Sengerema alifika katika jengo la Hospitali hiyo jua likiwa limezama na akafarijika kuona ujenzi wake unaendelea vyema ambapo Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.5 kwenye ujenzi huo.
Giza
halikumzuia Mongella aliyekuwa ameambatana na viongozi na watendaji mbalimbali
akiwemo Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mwl. Emmanuel Kipole, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Buchosa, Chrispian Luanda pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ngazi ya
Wilaya na Mkoa, kwani majira ya saa mbili kasorobo usiku, alihitimisha ziara
yake kwa akakagua ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Buchosa ambalo ujenzi wake
unagharimu shilingi Bilioni 2.5.
Wakazi Buchosa
wana matumaini makubwa na miradi hii pamoja na mingine mingi hivyo matarajio
yao ni kuona ikikamilika kwa wakati ili wapate huduma kikamilifu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwl. Emmanuel Kipole na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Buchosa, Chrispin Luanda.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: