STAMICO watakiwa kuutumia vyema mtambo wa kisasa wa kuchoronga miamba
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu
wa Madini, Prof. Simon Msanjila akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali
na Utawala, Nsajigwa Kabigi mara baada ya kuwasili katika ofisi za STAMICO kwa
ajili ya makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba. Katikati ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi, akieleza jambo kuhusu
mtambo huo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
(mwenye tai) na wajumbe walioshiriki katika tukio hilo.
Kutoka Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akifuatiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku pamoja na Msaidizi wa Katibu Mkuu
Justin Mdamila kabla ya makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba baina ya
wizara na Stamico.
Mtambo wa
kuchoronga miamba uliogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.3. Mtambo
huu unajulikana kama Multi-Purpose Air Rotary drill Rig.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi, (Kulia) akieleza jambo
mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili kulia)
kabla ya makabidhiano rasmi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi, akieleza jambo kuhusu
mtambo huo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
(mwenye tai) na wajumbe walioshiriki katika tukio hilo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Geo fields Tanzania Ltd Denis Dillip akizungumzia juu ya uwezo wa
mtambo huo. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon
Msanjila pamoja na ujumbe aliombatana nao.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (Kushoto) akimkabidhi Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku hati ya makabidhiano ya
mtambo wa kuchoronga miamba unaojulikana kama Multi-Purpose Air Rotary Drill
Rig.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akisalimiana na mmoja kati ya wajumbe
walioshiriki katika makabidhiano ya mtambo huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi pamoja na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku wakisaini hati za
makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi (Kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku wakionesha hati za
makabidhiano mara baada ya kusaini.
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutumia mtambo wa kuchoronga miamba kwa ufanisi ili kuliletea tija Taifa pamoja na shirika hilo kutokana na kipato kitakachotokana na uwepo wa mtambo huo.
Prof. Msanjila ameyasema hayo leo Desemba 24, 2018 wakati wa hafla fupi ya kuukabidhi rasmi mtambo huo kwa STAMICO kwa ajili ya kuanza kuutumia rasmi. Mtambo huo unaitwa Multi-Purpose Air Rotary Drill Rig.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Msanjila amesema, ununuzi wa mtambo huo ni uwekezaji mkubwa ambao Serikali imeufanya kwa shirika la Stamico hivyo, halina budi kuutumia vyema ili uweze kuleta tija.
Akizungumzia gharama za mtambo huo, Prof. Msanjila amesema umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki tatu(USD 1.3) ambazo yeye kama Mtendaji Mkuu wa wizara anaona kuwa na deni kubwa kwake, na hivyo kuahidi kuusimamia ipasavyo ili kuhakikisha mtambo huo unazalisha faida na kuwa chachu ya kuweza kununua mitambo mingine kama hiyo ili kukuza sekta ya madini nchini.
Aidha, amelitaka Shirika hilo kujitangaza vema ili wananchi na hususn wadau wa madini wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini kufahamu uwepo wa mtambo huo ili uweze kutumika hata kwa kampuni binafsi ili kujiongezea kipato lakini pia kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. “Kwa zabuni nilizozisikia mpaka sasa mtambo huu utazalisha pesa za kutosha” amesema Msanjila.
Mbali na kukabidhi mtambo huo, Prof. Msanjila ameitaka Stamico kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya mtambo huo kila robo ya mwaka ili kuweza kufanya tathmini endapo mtambo unatumika kwa faida.
Pia, ameliagiza shirika hilo kuhakikisha kuwa, mtambo huo unawezesha manunuzi ya mtambo mwingine mpya kila mwaka ili ndani ya miaka mitano shirika liweze kumiliki mitambo mitano na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini.
Akizungumzia ubora wa mtambo huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Geo field Tanzania Ltd Denis Dillip ambaye ndiye mnunuzi wa mtambo huo amesema, mtambo huo ni wa kisasa na unatumika katika kuchimba aina tatu za miamba lakini pia unaweza kutumika katika kuchimba visima vya maji.
Aidha, Denis ameishukuru Serikali kwa wazo la kununua mtambo huo na kukiri kuwa, utawasaidia wchimbaji wadogo katika kuendeleza kazi zao za uchimbaji na utafutaji wa madini.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylvester Ghuliku amekiri kuwa mtambo huo ni talanta waliyopewa na serikali na kuahidi kutoifukia na badala yake watahakikisha unatumika kwa faida na kuhakikisha unazalisha faida kwa serikali.
“Dola za kimarekani milioni 1.3 mlizotuamini na kutukabidhi ni pesa nyingi sana, na hamjatukabidhi ili zikae kwenye makabati, tutahakikisha tunautumia mtambo huu kwa weledi mkubwa ili uweze kuleta tija, ni imani yangu kuwa mtambo huu utanufaisha si Stamico pekee bali pia wachimbaji wadogo, wa kati, wakubwa na sekta nzima ya madini nchini,” amesema Ghuliku.
Ameongeza kuwa, mtambo huo unahitajika sana katika kufanikisha shughuli za utafutaji wa madini, hivyo atahakikisha katika kipindi cha mwaka mmoja stamico inazalisha ipasavyo kupitia mtambo huo na hivyo kuwezesha manunuzi ya mtambo mwingine wa aina hiyo.
No comments: