LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watoto waliozaliwa katika mkesha wa Krismas 2018

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Happy Msemwa (kulia) akizungumza jambo na Jane Mathias (30) mkazi wa Sinza aliyejifungua mtoto wa kiume usiku wa Disemba 25, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Jane Mathias (30) akimnyonyesha mtoto wake, Noel Alphonce baada ya kujifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa njia ya kawaida akifurahi na kumshukuru Mungu. "Nina kila sababu za kumshukru Mungu kwa kuniwezesha kumpata mtoto wa kiume kwa njia ya kawaida na nipende pia kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa huduma zao nzuri". Alisema Bi.Mathias.
Mkunga katika mafunzo taraji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Shukuru Siame akimpatia huduma, Asina Mkumba (29) mkazi wa Mbezi kwa Msuguri ambaye alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji katika Hospitalini hapo na kuzungumza na Muuguzi Mwandamizi Idara ya akina mama na watoto wachanga wa Hospitali hiyo, Mariam Mlawa. 

"Nashukuru Mungu watoto waliozaliwa katika usiku wa kuamkia mkesha wa Krismas Disemba 25, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni watano. Kati ya hao wawili walizaliwa kwa njia ya upasuaji, wakiume na wakike na kwa njia ya kawaida watatu, wawili wa kike na wa kiume mmoja na hali zao kwa ujumla zinaendelea vizuri. 

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Muuguzi wa zamu ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema "watoto waliozaliwa mkesha wa kuamkia Disemba 25, 2018 ni 12, wa kiume Tisa na wa kike wa tatu wakiwemo mapacha".
Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa Temeke, Hadija Kamote (kulia) akimwelekeza jambo Aisha Saiboko mkazi wa Maji Matitu Mbagala aliyejifungua kwa njia ya upasuaji usiku wa kuamkia mkesha wa Krismas katika Hospitali hiyo ambapo alijifungua mtoto wa kiume.
Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa Temeke, Hadija Kamote (kulia) akimsaidia Arafa Juma (27) jinsi ya kumbeba mtoto wakati akimnyonyesha watoto wake ambao walizaliwa katika mkesha wa kuamkia Disemba 25, 2018.
Na Khalifan Mussa

No comments:

Powered by Blogger.