LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ukeketaji bado pasua kichwa mkoani Mara

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Matangazo.

Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, Yassin Ally, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa Kijinsia katika wilaya ya Tarime mkoani Mara. Uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto na Wanawake katika kipindi cha mwaka 2017/22.

Uzinduzi huo ulifanyika Novemba 28, 2018 katika Kata ya Muriba ukienda sanjari na uzinduzi wa kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani. Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani ni kampeni ya Kimataifa  inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 kutokana na mauaji ya kinyama ya akina dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960. 

Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 kuwa siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa siku ya 16 ambayo ni Disemba 10 ya kila mwaka.
Picha na Frankius Cleoface, Tarime
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mara, Elizabert Mahinya, akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Tarime Glorious Luoga (hayuko pichani).
Baadhi ya wananchi wakiwa katika maandamano ya amani kufikisha ujumbe kuhusu jamii kuondokana na aina zote za vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwemo ukeketaji.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye maandamo hayo.
Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari walishiriki uzinduzi huo, lengo ikiwa ni kufikisha elimu kuhusu jamii kuondokana na aina zote za ukatili wa Kijinsia ikiwemo kwa watoto na wanawake.
Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia hufanyika kila mwaka kote duniani kufikisha elimu kwa jamii kuondokana na aina zote za vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
"Chapa Kazi, Siyo Mkeo"
"Kukeketa Sasa Basi"
Taswira ulipofanyika uzinduzi wa kampeni ya kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime.
Viongozi wa Serikali, Wanaharakati, Jesho la Polisi, Madiwani pamoja na Serikali za Mitaa walishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii. Kampeni hiyo ya Kitaifa inatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo shirika la KIVULINI katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Mara na Shinyanga.

Na BMG
Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara limetakiwa kutowafumbia macho wale wote watakaobainika kujihusisha na suala la Ukeketaji kwa watoto wa kike na badala yake kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Kauli hii imekuja wakati ambao baadhi ya wanajamii katika kabila la Wakurya mkoani Mara, wamejipanga kwa ajili ya kutekeleza mila potofu ya ukeketaji ambayo kwa kabila hilo hutekelezwa kila mwaka unaogawanyika kwa mbili.

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wasishana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, Yassin Ally alitoa rai hiyo Novemba 28, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake uliofanyika katika Kata ya Muriba wilayani humo.
Ally alisema vitendo vya Ukatili ikiwemo Ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni vinakwamisha kasi ya maendeleo katika jamii pamoja na kuchochea ufaulu hafifu kwa wanafunzi wa kike na hivyo kuwahimiza wazazi na walezi wilayani Tarime kujiepusha na vitendo hivyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Tarime Glorious Luoga, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa Mara, Elizabert Mahinya alisema kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu dhana ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na hivyo kuifikia Tarime Mpya isiyo ukatili.

Uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wakutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto unaotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 ambapo uzinduzi huo ulienda sanjari na kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani itakayofikia kilele chake Disemba 10.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.