LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyabiashara wa samaki waondolewa nje ya Soko Kuu Jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com 

Judith Ferdinand, BMG
Afisa Mfawidhi wa Ulinzi wa Raslimali za Uvuvi Kanda Kuu ya Ziwa Victoria, Didas Mtambalike amesema ni makosa kisheria wafanyabiashara wadogo wa samaki kufanya shughuli zao nje ya Soko Kuu Jijini Mwanza.

Mtambalike anasema soko la nje si rasmi kwa uuzwaji wa samaki na ni kinyume cha kanuni za afya na mazingira hivyo amewataka wote kurudi ndani kwenye eneo maalum lililotegwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya biashara hiyo.

"Suala hili halina siasa, hapa wote ni lazima mrudi ndani kufanya biashara kwenye eneo ambalo halmashauri imelitenga kwa ajili ya uuzaji samaki na majokofu yapo ili muyatumie wote, kuuzia samaki nje ya soko ni kinyume cha sheria na kanuni za afya na pia mazingira yake sio salama". Alisema Mtambalike na kubainisha kwamba zoezi la kuwaondoa nje wafanyabiashara hao wadogo litadumu kwa muda wa siku saba.

Aidha alisema kutokana na baadhi ya wafanyabishara kuuzia samaki nje ya soko, imesababisha walio ndani kukosa wateja na pia wamekua wakiuza samaki wachanga hivyo kupelekea wavuvi kuendelea na uvuvi haramu.

Florah Richard na Josephine Marko ambao ni miongoni mwa wauza samaki katika soko la nje walisema changamoto iliyopo ndani ya soko kuu ni wao kutakiwa kulipa shilingi 500,000 kwa mwezi kwa ajili ya meza huku mitaji yao ikianzia shilingi 50,000 hivyo hawawezi kumudu gharama hiyo ndiyo maana wamekimbilia nje.

Hata hivyo inaelezwa kwamba uongozi wa Soko Kuu Jijini Mwanza uliandika majina ya wafanyabiashara hao wadogo kwa ajili ya kuwapatia meza za bei nafuu ambazo watakuwa wanalipia shilingi 26,000 kwa mwezi wakiwa ndani ya soko.

No comments:

Powered by Blogger.