LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM wilayani Nyamagana ang'atuka rasmi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Charles Nyamasiriri (aliyesimama) amejiuzulu rasmi nafasi hiyo na kutoa fursa ya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya kufanyika.

Nyamasiriri alijiuzulu nafasi hiyo kwa mjibu wa Katiba ya CCM baada ya kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Isamilo katika uchaguzi mdogo uliofanyika Aprili 2018 ambapo uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti anayechukua nafasi hiyo unafanyika hii leo katika ukumbi wa "Gand Hall" Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.