LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella avutiwa na shamba la kuku la "SMJ Poultry Egg Farm" wilayani Magu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametembelea shamba la kisasa la kuku wa mayai la "SMJ Poultry Egg Farm" lililopo wilayani Magu, lililoanzishwa na mbunge wa jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor kwa mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akiwa katika shamba hilo, Mongella amempongeza mbunge Mansoor kwa uwekezaji huo unaoenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano ya Uchumi wa Viwanda na kumuahidi kwamba atashirikiana na viongozi wengine katika kuimarisha upatikanaji wa soko la mayai.
Mkurugenzi wa mradi wa kuku wa SMJ Poultry Egg Farm, Shanif Mansoor ambaye pia ni Mbunge wa Kwimba (mwenye nguo nyekundu), akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi wa kuku wa SMJ Poultry Egg Farm.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akimpongeza Mkurugenzi wa mradi wa kuku wa SMJ Poultry Egg Farm, Shanif Mansoor ambaye pia ni Mbunge wa Kwimba (kushoto), kwa uwekezaji mkubwa alioufanya. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Magu, Hilal Elisha (wa pili kushoto).
Tazam BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.