LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Kwimba awekeza zaidi ya bilioni moja kwenye kuku

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (CCM) ametumia zaidi ya shilingi bilioni moja kuwekeza katika shamba la kisasa la ufugaji wa kuku wa mayai katika eneo la Nyanguge wilayani Mwanza.

Mansoor ambaye ni Mkurugenzi wa shamba hilo liitwalo SMJ Poultry Egg Farm anafafanua kuhusiana na uwekezaji huo mkubwa mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyemtembelea, Januari 11, 2019.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akipata ufafanuzi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor (wa pili kulia) kuhusiana na mradi wake wa ufugaji kuku wa mayai.
Mashine za kuandaa chakula cha kuku.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (mwenye nguo nyekundu) akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wake wa ufugaji wa kuku kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (mwenye kofia), aliyeambatana pia na Mkurugenzi Halmashauri ya Magu, Lutengano Mwalwiba (kulia), Mkuu wa Wilaya Magu Dkt. Philemon Sengati (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Magu, Hilal Elisha (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi wa kuku SMJ Poultry Egg Farm.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.