LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waliomsaidia mama kujifungua mapacha wanne wasimlia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure ambao walimsaidia mama Jenipher John (23) mkazi wa Ibanda Manispaa ya Ilemela kujifungua mapacha wanne Januari 09, 2019 majira ya saa saba mchana wameeleza mwanzo mwisho shughuli hiyo ilivyokuwa.

Mama huyo ambaye mimba yake ya kwanza pia ilikuwa ya mapacha wanne japo Aprili 2018 iliharibika ikiwa na miezi sita, anaiomba serikali kumsaidia kulea watoto hao kwani peke yake hawezi kwa kuwa hana shughuli ya kumuingizia kipato huku mme wake anayefanya kazi ya kuendesha pikipiki (bodaboda) akiwa na uchumi wa kawaida.

No comments:

Powered by Blogger.