LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella amjulia hali mama aliyejifungua mapacha wanne

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) amemtembelea mama Jenipher John (23) mkazi wa Ibanda Manispaa ya Ilemela aliyejifungua watoto wanne Januari 09, 2019 majira ya saa saba mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Sekou Toure.

Mama huyo ambaye mimba yake ya kwanza iliyokuwa na mapacha wanne iliharibika ikiwa na miezi sita, anaiomba serikali kumsaidia kulea watoto hao kwani peke yake hawezi kwa kuwa hana shughuli ya kumuingizia kipato huku mme wake anayefanya kazi ya kuendesha pikipiki (bodaboda) akiwa na uchumi wa kawaida.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Christopher Gachuma akimpongeza Jenipher John aliyejifungua watoto wanne katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Christopher Gachuma (kushoto) wakimpongeza Jenipher John aliyejifungua watoto wanne katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Christopher Gachuma (katikati) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu Benki ya CRDB, Dkt Joseph Witts (kushoto), wakimpongeza Jenipher John aliyejifungua watoto wanne katika hospitali hiyo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.