LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella ashuhudia makabidhiano ya kiwanda cha Mwanza Tanneries

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameshuhudia makabidhiano ya kiwanda cha ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo wilayani Ilemela, yaliyosainiwa na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio (kushoto) pamoja na Msajili wa Hazina, Athuman Mbuttuka (kulia), hii leo Januari 10, 2018.

Serikali mkoani Mwanza chini ya Mkuu wa Mkoa John Mongella ilikirejesha kiwanda hicho mikononi mwake baada ya mwekezaji aliyekuwa amekabidhiwa kushindwa kukiendeleza hivyo imekikabidhi kwa Msajili wa Hazina kwa ajili ya hatua nyingine ya kukikabidhi kwa mwekezaji atakayekuwa tayari kukiendeleza/ kutumia eneo la kiwanda hicho.

Awali kiwanda hicho kilikuwa kinamilikiwa na kampuni ya Afrika Tanneries kisha kubadilishwa umiliki kwenda kampuni ya Kasco ambapo Julai 2017 kilirejeshwa serikalini baada ya kusimama kufanya kazi kwa muda mrefu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio (kushoto) pamoja na Msajili wa Hazina, Athuman Mbuttuka (kulia), wakisaini makubaliano ya makabidhiano ya kiwanda cha ngozi cha Mwanza Tanneries.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.