LIVE STREAM ADS

Header Ads

+VIDEO: Wagombea Jumuiya ya Wazazi CCM wilayani Nyamagana wakijinadi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Dismas Masunu ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, akitoa ufafanuzi kabla ya wagombea wa nafasi hiyo kujinadi na wajumbe kupiga kura.

Uchaguzi huo unafanyika leo katika ukumbi wa "Gand Hall" Jijini Mwanza baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Charles Nyamasiriri kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Isamilo katika uchaguzi mdogo uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kujiuzulu kwa mujibu wa Kanuni za CCM za uchaguzi za mwaka 2017 ambapo zinataka mtu mmoja kuwa na nafasi moja ya uongozi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwashum Ismail ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, akisoma kanuni za uchaguzi kabla ya wagombea wa nafasi hiyo kujinadi na wajumbe kupiga kura.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakijitambulisha mbele ya wajumbe. Kutoka kushoto ni Joseph Kadege Bupamba, Mashaka Kamchape Kaguna pamoja na Peter John Bega.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakijitambulisha mbele ya wajumbe. Kutoka kushoto ni Joseph Kadege Bupamba, Mashaka Kamchape Kaguna (katikati) pamoja na Peter John Bega (kulia).
Wajumbe wa Mkutano wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.