LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa awatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Same

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jesca Mbogo (kulia), akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Same mkoani Kilimanjaro baada ya kuwasili mkoani humo, jana Januari 23, 2018 ikiwa ni mkoa wake wa pili baada ya Tanga katika mwendelezo wa ziara zake katika mikoa mbalimbali nchini.
BMG Habari
Baadhi ya wagonjwa wakiwemo akina mama wanaopata matibabu katika Hospitali ya Wilaya Same walimshukru Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo kwa msaada huo na kumuomba awafikishie salamu kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa juhudi zake za kuboresha sekta ya afya nchini kwani hizi sasa wananchi wanapata huduma bora za afya.
Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akiwa amembeba mmoja wa watoto katika Hospitali ya Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Powered by Blogger.