LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Afya ambana mkandarasi ujenzi wa Hospitali mkoani Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joel Maduka, Geita
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema haridhishwi na kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita na hivyo kumtaka mkandarasi kuongeza juhudi ila kukamilisha ujenzi huo kwa wakti ifikapo Julai 2019.

Waziri Mwalimu aliyasema hayo baada ya kufanya ziara katika mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Hata hivyo Msimamizi wa mradi huo, Grace Elias alijitetea kwamba sababu mbalimbali ikiwemo mvua zimesababisha kasi ya ujenzi wake kusuasua.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.