LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko apiga marufuku uchimbaji madini katika Hifadhi ya Makao mkoani Simiyu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amepiga marufuku shughuli za uchimbaji madini ya ujenzi pamoja na utafiti wa madini ya shaba katika Hifadhi ya Wanyama ya Jamii (WMA) Makao iliyopo Wilaya ya Meatu mkoani Simiu.

Biteko alipiga marufuku hiyo Januari 05, 2018 alipofanya ziara katika hifadhi hiyo akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tume ya Madini.

Hatua hiyo inajiri kufuatia taarifa za baadhi ya watu kuanza kufanya utafiti wa madini ya shaba katika pori hilo kinyume cha sheria huku kampuni ya uwindaji ya Mwiba Holdings ikiwa tayari imepigwa faini ya Shilingi Milioni 50 kwa kuchimba madini ya ujenzi katika hifadhi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.