LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHUKRANI MUSIC CONCERT: RC Mongella alivyompandisha Mr. Blue jukwaani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wakazi wa Jiji la Mwanza wamefurahia burudani kali kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mr. Blue kwenye tamasha la wazi la “Shukrani Music Concert” lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano Halotel ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.

Katika tamasha hilo lililofanyika Januari 12, 2018 kwenye uwanja wa Furahisha, kampuni ya Halotel ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake ikiwemo fulana na simu. Pia Halotel iliyoanza kutoa huduma zake nchini tangu Oktoba 15, 2015 ilitoa mashuka 50 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na mengine 50 katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukerewe. Pia ilitumia zaidi ya shilingi Milioni Sita kununua madawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Bwisya pamoja na Hospitali ya Sekou Toure.

Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambapo mbali na kuishukru kampuni ya Halotel kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini, pia alimpandisha jukwaani kwa shangwe msanii Mr. Blue.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye tamasha hilo.
Msanii Mr. Blue akipafomu kwenye tamasha hilo.
Shukrani Music Concert Jijini Mwanza
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.