UWT Mwatulole mkoani Geita watoa pedi kwa wanafunzi wa kike
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joel Maduka, Geita
Umoja wa Wanawake
wa Chama cha Mapinduzi (UWT), tawi la Mwatulole Kata ya Buhala mkoani Geita,
wamekabidhi taulo la zike (pedi) kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya
Sekondari Mwatulole.
Mwenyekiti
wa tawi hilo, Rosemary Michael amesema taulo hizo zilipatikana kufuatia
kongamano la wanawake lililofanyika hivi karibuni Mjini Geita na kwamba
zitawasaidia wanafunzi wa kike wanaotoka katika familia zisizojimudu vyema
kiuchumi na hivyo kuondokana na changamoto ya kukosa masomo wakati wa mzunguko
wao wa hedhi.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: