LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Songwe aitaka TBA kukamilisha miradi kwa wakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Katibu Tawala Mkoa Songwe, David Kafulila akisaini mikataba ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa Songwe na ya Katibu Tawala Mkoa Songwe ambapo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameahidi kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
Katibu Tawala Mkoa Songwe, David Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa Songwe, Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa Songwe na Katibu Tawala Mkoa Songwe. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Mkoa Songwe, Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.

Ofisi ya RAS Songwe
Mkuu wa Mkoa Songwe, Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Tanzania (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (Rtd) Mwangela ameyasema hayo wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa Songwe na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa Songwe kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa Songwe.

"TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi". Alieeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Aliongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila aliishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Kafulila alisema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa Songwe, Mhandisi Fidelis Cosmas pia aliishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas alisema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.

No comments:

Powered by Blogger.