LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Mwanza aongoza mapokezi ya madaktari bingwa kutoka nchini Cuba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati), akiongoza ujio wa madaktari bingwa saba kutoka nchini Cuba baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kutoa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando. 

Madaktari bingwa wengine wanne kutoka nchini Cuba wanatarajiwa kuwasili Jijini Mwanza hivi karibuni kuungana na wenzao ambapo mbali na kutoa huduma za afya kwa wananchi, pia watasaidia kuwajengea uwezo madaktari wazawa katika Hospitali ya Rufaa Bugando.

Viongozi wengine ni, Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (kushoto) pamoja na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio (kulia).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akimlaki Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa ameambatana na madaktari bingwa saba kutoka Cuba. Anayeshuhudia kulia ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Christopher Kadio.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akimlaki kiongozi wa msafara wa madaktari bingwa saba kutoka nchini Cuba, Dkt. Juan Arias (kushoto), baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Profesa Abel Makubi akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akimlaki kiongozi wa msafara wa madaktari bingwa saba kutoka nchini Cuba, Dkt. Juan Arias (kushoto), baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Profesa Abel Makubi akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (katikati).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza jambo wakati wa mapokezi hayo.
Mapokezi ya madaktari bingwa saba kutoka nchini Cuba katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (katikati), akifanya utambulisho wa madaktari bingwa sana waliowasili Jijini Mwanza wakitokea nchini humo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kulia ni kiongozi wa msafara wa madaktari bingwa saba kutoka nchini Cuba, Dkt. Juan Arias.
Utambulisho wa madaktari bingwa saba kutoka Cuba waliowasili Jijini Mwanza ukifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (wa tatu kulia), madaktari bingwa saba kutoka nchini kubwa na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), akimpongeza Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hermandez Polledo (wa tatu kulia), kwa kuendeleza ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Cuba.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.