LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAA kuchunguza kwa nini wafanyabiashara wanatumia viwanja vya nje

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), akizungumza jana baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Natures Fish Limite kilichopo Jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mamaka ya viwanja vya ndege nchini (TAA) imesema itafanya uchunguzi ili kubaini sababu za baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo wenye viwanda vya kuchakata minofu ya samaki kutumia viwanja vya ndege vya nchi jirani kusafirisha mizigo yao badala ya kutumia viwanja vya ndani.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Richard Mayongela aliyasema hayo jana kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ya kutembelea viwanda vya kuchakata mabondo na minofu ya samaki Jijini Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.