Biteko afunguka kwa uchungu mkubwa mbele ya Makamu wa Rais
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu wa
Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan jana ameendelea na ziara yake mkoani
Tabora kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na
wananchi katika Wilaya za Uyui pamoja na Nzega.
Akiwa katika
Wilaya ya Uyui, Mama Samia alikagua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa
Kituo cha Afya Igalula na pia kuzungumza na wananchi ambapo kwa Wilaya ya
Nzega, alikagua upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora (Kitete) unaogharimu shilingi Milioni
800, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha gesi cha Mara Moja
Construction.
Pia alizungumza
na wanachi kupitia mkutano wa hadhara katika Kata ya Puge na baadae kushiriki
mazishi nyumbani kwa mbunge wa Nzega ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyefiwa
na mtoto wake.
Katika ziara
hiyo iliyoanza juzi mkoani Tabora, Mama Samia aliambatana na viongozi
mbalimbali wakiwemo Mawazili pamoja na Manaibu Mawaziri na hapa Waziri wa
Madini, Doto Biteko alipata fursa ya kutoa salamu za wizara hiyo (video iko mwishoni).
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda mche wa mti baada ya kukagua upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora, Kitete.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pia aliungana na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kushiriki mazishi ya mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbunge wa Nzega) yaliyofanyika nyumbani kwake Puge.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: